Jumanne , 6th Apr , 2021

Mcheza kikapu wa timu ya Dallas Mavericks, Luka Doncic amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa wiki ya 15 kwenye ligi kuu ya kikapu nchini Marekani kwa upande wa Magharibi baada ya kuonesha kiwango safi kilichoifanya timu yake kushinda michezo mitano mfululizo.

Luka Doncic wa Dalla Mavericks (kushoto) na Jrue Holiday wa Milwaukee Bucks (kulia).

Doncic amewapiku wacheza kikapu wenzake wote wa upande wa Magharibi kwa kuwa na wastani wa kufikisha alama 28.3, rebaundi 6.6 na kutengenza mabao 6.3 na kushinda michezo 4 mfululizo iliyochezwa kunzia wiki ya tarehe 29 Machi 2021 hadi Aprili 3 mwaka huu.

Kwa upande wa Jrue Holiday wa timu ya Milwaukee Bucks amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo wa wiki ya 15 kwa upande wa mashariki baada ya kufikisha wastani wa alama 26.8, rebaundi 8.5 na wastani 62.7 wa kufunga mabao uwanjani na kusaidia timu yake kushinda michezo mitatu.

NBA inataraji kuendelea tena alfajiri ya kuamkia kesho kwa michezo 8 huku ule unaosubiriwa kutazamwa na wengi ni mchezo wa mabingwa watetezi Los Angeles Lakers watakaocheza na mabingwa wa msimu juzi timu ya Toronto Raptors.