Jumatano , 18th Oct , 2017

Klabu ya soka ya Borussia Dortmund huenda ikawa timu ya kwanza inayoongoza ligi ya nyumbani kwenye ligi tano bora duniani kuaga mapema michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Dortmund imelazimishwa sare ya bao 1-1 na APOEL Nicosia nakufanya ikose ushindi kwenye mechi zake tatu za hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya mechi mbili za awali kupoteza dhidi ya Real Madrid na Tottenhm.

Timu hiyo kutoka Ujerumnai inaongoza Bundesliga ikiwa na alama 19, imeshindwa kuonesha makali yake kwenye UEFA ambapo sasa ipo nafasi ya 3 kwenye kundi H ikiwa na alama 1 nyuma ya mabingwa watetezi Real Madrid wenye alama 7 sawa na Tottenham ambayo inashaika nafasi ya pili.

Dortmund sasa italazimika kushinda mechi zake zote tatu za marudiano dhidi ya Real Madrid na Tottenham huku ikiomba timu hizo zifungwe na APOEL Nicosia. Zaidi ya hapo timu hiyo itakuwa imejiondoa rasmi kwenye michuano hiyo.