Ijumaa , 18th Sep , 2020

Ligi kuu ya England EPL ni ligi bora na yenye mvuto Duniani na hii inatajwa kuwa ni moja ya sababu kubwa inayowafanya wachezaji wengi kuwa na ndoto ya kucheza katika ligi hiyo tajiri zaidi.

Kai Havertz kulia akiwa na kocha wa Chelsea Frank Lampard kudhoto, Kai amejiunga na Chelsea akitokea Bayer Leverkusen ya Ujerumani

Kila msimu mpya wa mashindano unapoanza huwa tunashuhudia timu za EPL zikisajili wachezaji bora wa madaraja ya juu ( world class player ) kutoka katika ligi mbali mbali ikiwa katika harakati za kuboresha vikosi vyao.

Timu za England zimekuwa zikitumia pesa nyingi kununua wachezaji wa madaraja ya juu kutokana na jeuri ya kiuchumi walionaye kwani ligi kuu yao ndio ligi tajairi zaidi Dunia.

Ligi kuu ya Ujurumani (Bundesliga) ni moja ya Ligi ambayo imekuwa ikiwapoteza wachezaji wake bora ambao wamekuwa wakisajiliwa na vilabu vya ligi kuu england EPL.

Moja kati ya wachezaji bora kwenye EPL kwa sasa ni kiungo wa Manchester City Kevin De Bruyne ambaye alijiunga na Man city mwaka 2015 akitokea Wolfsburg ya Ujerumani, na amekuwa akitajwa na vyanzo vingi kuwa ni kiungo bora mchezeshaji katika soka la kisasa kuwahi kuonekana nchini England.

 

Nyota wengine walisajiliwa kutoka Bundesliga na wanafanya vizuri kwenye ligi kuu England EPL ni pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wa Arsenal ambaye alijiunga na The Gunners mwaka 2018 akitokea Borusssia Dortmund, mshambuliaji wa Tottenham Heung-Min Son alitokea Bayer Leverkusen, Roberto Firmino mshambuliaji wa Liverpool alijiunga na majogoo akitokea Hoffenheim.

Kevin Debruyne kiungo wa Manchester City ni moja kati ya wachezaji bora kwenye ligi kuu England EPL, alijiunga na Manchester City mwaka 2015 akitokea Wolfsburg ya Ujerumani

Msimu huu pia wa 2020-21, EPL hauijawaacha tena salama Bundesliga kwani imewasajili baadhi ya wachezaji waliofanya vizuri kwenye Ligi kuu Ujerumani Bundesliga msimu uliopita ambao ni.

Timo Werner mshambulliaji wa kimataifa wa Ujerumani amejiunga na Chelsea akitokea RB Leipizing na Chelsea imelipa ada ya uhamisho ya fedha za Uingereza pauni milioni 47.7 amabayo ni taklibani bilioni 110 za kitanzania.

Ukichangiza na umri wake wa miaka 24 anatajwa kuwa moja kati ya washambuliaji hatari vijana barani Ulaya kwa sasa, ubora wake kiufundi, spidi, mikimbio hatari kwenye eneo la timu pinzani na uwezo wake wa kufunga anatajwa anataegemewa kuwa moja kati ya washambuliaji hatari Duniani kwa miaka ijayo.

Msimu uliopita akaiwa na kikosi cha Leipzing alifunga jumla ya mabao 34 kwenye michezo 45 kwenye mashindano yote huku mabao 28 kati ya hayo alifunga kwenye michezo ya ligi kuu Bundesliga.

Kai Havertz kipaji kingIne kikubwa kilicho vushwa kutoka ardhi ya Ujerumani mpaka England Chelsea wamelipa dau la ada ya uhamisho ya fedha za uingereza pauni milion 72 kwa Bayer Leverkusen ambayo ni zaidi ya bilioni 167 za kitanzania kwa kijana huyu wa kijerumani mwenye umri wa miaka 21.

Kiufundi anatajwa kuwa anakipaji cha asili (gifted) uwezo wake wa kutumia miguu yote uwezo wa kuulinda mpira na jicho la kupiga pasi kwa usahihi na uwezo wa kufunga. Akiwa na umri wa miaka 19 uwezo wake ulifananishwa na Mesut Ozil kiungo wa Arsenal na zamani timu ya taifa ya Ujerumani.

Kadri alivyozidi kucheza akatajwa aina yake ya uchezaji inafanana na ile ya kiungo gwiji wa zamani wa kijerumani Michael Ballack na Toni Kroos wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ujerumani kufananishwa na wachezaji wengi bora wanao cheza katika eneo la kiungo Kai Havertz anatajwa kama ni kiungo mwenye uwezo wa kufanya vitu vyote.

 

Msimu ulipita akiwa na kikosi cha Leverkusen mabao 18 katika michezo 45 ambapo kwenye ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga alifunga mabao 12 na pasi za usaidizi wa mabao (Assists) 6 katika michezo 30 na alikuwa katika kikosi kilichoanza alianza katika michezo 29.

Mwingine ni Thiago Alcantara kutoka Bayern Munich amejiunga na kikosi cha mabingwa wa England Liverpool kwa mkataba wa miaka 4 kwa ada ya uhamisho ya fedha za uingereza pauni milion 25 zaidi ya bilioni 74 za kitanzania.

Ni mchezaji mshindi katika misimu yake 7 aliyoitumikia the Bavarians ameshinda jumla ya mataji 16, akiwa na umri wa miaka 29 anatajwa kuwa anakuja kuongeza uzoefu na hali ya ushindi kwenye kikosi cha Kocha Jorgen Klopp.

Ni mchezaji fundi na mbunifu huyu ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Manzinho.

Thiago katika maisha yake ya soka amekuwa akimtazama Ronaldinho kama mchezaji wake wa mfano yani (role model) lakini kulelewa kwake kisoka katika kituo cha FC Barcelona La Masia akiwaona Xavi na Iniesta moja kati ya viungo bora inatajwa kuwa amejifunza mengi na ndio maana ameonekana kuwa fundi mnoo.

Sio mzuri sana kwenye kufunga msimu uliopita alifunga mabao 3 tu kwenye michezo 40 kwenye mashindano yote na hakuna Assists. Lakini huyu ni mchezaji anayekuja kuongeze ubunifu kwenye kiungo cha liverpool msimu uliopita alikuwa na wastani wa kutengeneza nafasi moja ya kufunga kila baada ya dakika 90.

Huu ni ubora ambao vilabu vya Ligi kuu England EPL wameuamisha kutoka Bundesliga kwa msimu huu mpya wa mashindani wa 2020-21 kubwa tunasubiri tuone kama watafanikiwa kufikia matarajio ya wadau na mashabiki.