Jumamosi , 14th Oct , 2017

Wacheza Tennis wawili bora duniani, namba moja Rafael Nadal na namba mbili Roger Federer, watakutana katika fainali ya Shanghai Masters baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali leo.

Rafael Nadal mapema leo alimshinda Mcoratia Marin Cilic kwa seti 7-5 7-6 (7-3) katika mchezo uliodumu kwa saa mbili na dakika 11.

Roger Federer naye amefanya vizuri kwenye nusu fainali yake baada ya kumshinda Muargentina Juan Martin del Potro kwa seti 3-6 6-3 6-3 chini ya masaa mawili.

Bingwa wa Wimbledon Federer alimpiga Nadal na kushinda Michuano ya wazi ya Australia mwezi Januari na kushinda mechi nne za mwisho walizokutana wachezaji hao wawili ambao wote wameshinda Grand Slams 35 kila mmoja