Jumatatu , 18th Sep , 2017

Golikipa wa Azam FC Benedict Haule amekosa programu ya mazoezi ya leo asubuhi chini ya mwalimu Aristica Cioaba kufuatia maumivu ya kidole Gumba.

Msemaji wa Azam FC Jafar Idd Maganga amethibitisha taarifa hiyo japo kuwa ameshindwa kueleza ni muda gani atatumia kujiuguza. Jafar amesema kesho Septemba 19 ndio atatoa taarifa kamili kuhusu majeruhi ya Haule baada ya daktari kuwa amemfanyia vipimo na kujua undani wa tatizo.

"Siwezi kusema lolote kwasasa hadi kesho daktari wa timu atakapotoa ripoti ya tatizo la Benedict Haule", amesema Jafar. Azam imeendelea na mazoezi yake leo asubuhi ikijiwinda na mchezo wa Jumapili Septemba 24 kwenye uwanja wa Azam Complex dhidi ya Lipuli FC ya Iringa.

Wachezaji wengne ambao ni majeruhi ndani ya kikosi cha Azam FC ni Joseph Kimwaga na Shaaban Idd.ambao wanaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini.