Ijumaa , 20th Oct , 2017

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amethibitisha kuwa mshambuliaji Sergio Aguero amepona na yupo tayari kucheza mchezo wa kesho dhidi ya Burnley.

Akiongea leo kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho Guardiola amesema kikosi chake kipo vizuri lakini kinatakiwa kuendelea kuwa bora kila siku licha ya kukiita “Kikosi kilichokamilika” baada ya ushindi wa Jumanne dhidi ya Napoli.

“Timu yangu iko vizuri na tayari kwa mchezo wa kesho, lakini tunatakiwa kuendelea kuwa bora ili kufikia malengo, kuwa kikosi kilichokamilika haimanishi tusiongeze juhudi”, amesema Guardiola.

 “Aguero amepona tangu mechi ya Stoke City lakini hakupata muda zaidi wa kufanya mazoezi ndio maana hakucheza ila kwasasa yupo tayari kucheza, ila timu itaendelea kumkosa nahodha Vicent Kompany kwasababu bado ni majeruhi”, amesema Guardiola.

Manchester City inaongoza msimamo wa EPL ikiwa na alama 22 baada ya mechi nane ikiwa mbele kwa pointi mbili dhidi ya Manchester United yenye alama 20.