Jumanne , 21st Nov , 2017

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola, amegomea sifa na kusema timu yake bado haistahili sifa za kuwa miongoni mwa timu zenye nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kuelekea mchezo wao wa hatua ya makundi dhidi ya Feyenoord leo, Guardiola amesema anaheshimu timu yake kutajwa kama moja ya timu bora duniani kwasasa lakini ukweli ni kwamba hizo ni sifa tu ila hawajafanya chochote hadi sasa na ili kudhibitisha wanahitajika kushinda mataji.

“Tunajitahidi kucheza vizuri na tunaheshimu kutajwa kama timu bora lakini lazima tushinde mataji ili tufikie ukubwa wa timu zingine barani Ulaya kama Bayern Munich, FC Barcelona na Real Madrid”, amesema Guardiola.

 

Manchester City haijapoteza mechi hata moja kwenye michezo 18 iliyocheza msimu huu ikiwa tayari imeshafuzu katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya. Timu hiyo pia inaongoza ligi kuu ya England ikiwa na alama 34.