Jumatatu , 23rd Oct , 2017

Lewis Hamilton wa Mercedes ameshinda mbio za magari za Marekani (USGP) na kuongeza wigo wa pointi dhidi ya mpinzani wake Sebastian Vettel wa Ferrari kuelekea mwishoni mwa msimu wa 2017.

Hamilton sasa anasubiri mbio zijazo za Mexico Grand Prix na kama atashinda kwa tofuati kubwa dhidi ya Vettel basi atatwaa taji lake la nne la dunia. Togfauti na hapo itabidi kusubiri hadi mbio za Brazil au za mwisho Abu Dhabi ili kuweza kujihakikishia ubingwa pamoja na kuwa yupo kwenye nafasi nzuri zaidi.

Msimu huu umekuwa mzuri kwa Muingereza huyo ambapo hadi sasa anamzidi Vettel kwa alama 66 baada ya kushinda mbio za usiku wa jana huku Vettel, akimaliza wa pili. Hamilton sasa anadaiwa pointi 9 tu kwa na tofauti ya  alama 75 ambazo zitamwezesha kuwa bingwa wa msimu kwani Vettel hatowezi kuzifikia.

Ili kufufua matumaini ya ubingwa kwa Vettel wa Ferrari anapaswa kumzidi Hamilton kwa alama 17 kwenye mbio za Mexico Oktoba 27 – 29 mwaka huu vinginevyo Hamilton atatangazwa bingwa. Ili Vettel amzidi Hamilton pointi 17 basi anapaswa kushinda mbio hizo huku Hamilton akimalza nafasi ya sita au zaidi kitu ambacho ni kigumu kutokana na ubora wa Hamilton msimu huu.

Baada ya mbio za jana timu ya Lewis Hamilton amefikisha alama 331 huku mpinzani wake Sebastian Vettel wa Ferrari akifikisha alama 265. Endapo Hamilton atashinda ubingwa msimu huu basi itakuwa ni mara ya nne mfululizo kwa Mercedes na ya pili kwa Hamilton ndani ya misimu minne.