Jumamosi , 23rd Jul , 2016

Nahodha wa Klabu ya Yanga Nadir Haroub Cannavaro amesema, mchezo wa marudiano dhidi ya Medeama ni mgumu lakini ushindi pia kwa upande wao ni lazima ili kuweza kujiweka katika hali ya usalama katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrik

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' (kushoto), beki Andrew Vicent 'Dante' (Katikati) na kulia ni Kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima wakiwa Uwanja wa Ndege jijini Dar es salaam.

Cannavaro amesema, licha ya kupoteza michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja lakini hawawezi kukata tamaa katika safari ya kuwania kusonga mbele katika michuano hiyo kwani bado wanaamini nafasi ipo.

Cannavaro amesema, kocha ameangalia mapungufu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita na ameyafanyia marekebisho ili kuweza kukiweka kikosi katika uimara zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano siku ya jumanne.

Yanga imeondoka Alfajiri ya leo kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya timu ya Medeama utakaopigwa jumanne ya Julai 26 mwaka huu nchini humo.