Jumapili , 15th Oct , 2017

Kamati ya Dharura ya Shirikisho la Soka Barani Afrika, ikiongozwa na Rais Mr. Ahmad, imekutana Oktoba 14, 2017 huko Lagos, Nigeria, na kwa pamoja imeamua kutoa nafasi kwa nchi ya Morocco kuandaa fainali za tano za CHAN.

Uamzi huo umekuja muda mfupi baada ya nchi ya Kenya  kupokonywa nafasi hiyo tarehe 23 Septemba 2017 kwenye mkutano wa CAF uliofanyika huko Accra, Ghana, ambao ulibaini kasoro kadhaa ikiwemo kuchelewa kukamilika kwa maadalizi.=

Baada ya Kamati ya Utendaji ya CAF kujiridhisha kuwa mwendendo wa maandalizi ya Kenya kulingana na muda wa mwisho uliotolewa haijafikia malengo ndipo ikaunda kamati ya dharura ili kufanya mchakato wa zabuni ya kuchagua nchi mpya.

Nchi ambazo zilikuwa zinashindana na Morocco kuwania nafasi hiyo ya uenyeji wa Kombe la Mataifa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ikifahamika kama CHAN ni Equatorial Gueine na Ethiopia.

Fainali hizo za CHAN 2018, zimepangwa kuanza Januari 12 na kumalizika Februari 4, 2018. Jumla ya mataifa 16 yatachuana kuwania taji hilo ambapo Tanzania ilitolewa na Rwanda.