Ijumaa , 20th Mei , 2022

Kikosi cha wachezaji 28 wanatarajiwa kuingia kambini Mei 28 kujiandaa na michezo ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast huku viungo Himid Mao kutoka klabu ya Ghazi Mahl-Misri na Salum Abubakari ‘Sure Boy’ wa Yanga wakiwa ni miongoni mwa maingizo mapya Stars

Himid Mao kutoka klabu ya Ghazi Mahl-Misri na Salum Abubakari ‘Sure Boy’ Yanga.

Stars inaingia rasmi kambini Mei 28 kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu AFCON dhidi ya Niger utakaopigwa nchini humo Juni 4 kisha watacheza na Algeria Juni 8 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji hawa awali hawakujumuishwa kwenye kikosi kilichocheza mechi ya za kirafiki za kalenda ya FIFA.

Akizungumzia kuitwa kwa wachezaji hao, kocha msaidizi wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Shadrack Nsajigwa amesema sababu ya kuitwa kwa wachezaji hao ni kutokana na viwango wanavyovionyesha kwenye klabu zao.

“Mao na yeye licha ya awali alikuwa haitwi safari hii tumemuita kwa sababu watu wetu wamemfuatilia anachokifanya na kulizika na uwezo wake,” amesema Nsajigwa

Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula, Abuutwalib Mshery, Metacha Mnata, Shomari Kapombe, Kibwana Shomari, Haji Mnonga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala ‘ na Nickson Kibabage.

Wengine ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Kennedy Juma, Abdallah Kheri ‘Sebo’, Novatus Dismas na Mzamiru Yassin.

Wengine ni Aziz Andambwile, Himid Mao, Simon Msuva, Kelvin John, Mbwana Samatta, Farid Mussa na Abdul Suleiman.

Wengine ni Feisal Salum, Ben Starkie, Reliants Lusajo, Kibu Denis, George Mpole, Salum Abubakari ‘Sure Boy’ na Ibrahim Joshua.