Alhamisi , 17th Sep , 2020

Chama cha Soka Nchini Ufaransa kimetoa adhabu kwa waliohusika na vurugu katika mchezo wa Ligi Kuu kati ya PSG na Marseille iliomalizika kwa wachezaji watano kutolewa Uwanjani kwa kadi nyekundu.

Neymar JR Akizozana na mwamuzi wa mchezo uliozikutanisha PSG na Marseille wiki iliyopita.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji waliofungiwa

-Layvin Kurzawa amefungiwa mechi 6

-Jordan Amavi amefungiwa mechi 3

-Neymar JR amefungiwa mechi 2

-Leandro Parede amefungiwa mechi 3

-Dario Benedetto amefungiwa mechi 1

Vilevile LFP linafanya uchunguzi kubaini ukweli wa malalamiko ya Neymar juu ya kufanyiwa ubaguzi wa rangi na Alvaro Gonzalez.

Pia LPF linachunguza kama Angel di Maria alimtemea mate Alvaro Gonzalez.

MECHI ATAKAZOZIKOSA NEYMAR

NICE V PSG-Tarehe  20/09

REIMS V PSG-Tarehe  27/09