Jumatatu , 30th Nov , 2020

Klabu ya Azam Fc itashuka dimbani jioni ya leo huko mkoani Mara itakapokaribiana na Biashara ikiwa ni muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Mshambuliaji wa Azam Fc, Prince Dube (Pichani) atakosekana katika mchezo wa leo dhidi ya Biashara kutokana na kuumia mkono na ameelekea Afrika Kusini kupata matibabu zaidi.

Kikosi cha Azam kitakuwa kikiongozwa na kocha Vivier Bahati ambaye amekabidhiwa mikoba iliyoachwa na Aristica Cioba ambaye alifutwa kazi kufuatia mwenendo mbovu wa kikosi hicho.

Azam Fc walio katika nafasi ya pili wakiwa na alama 25, watakuwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 walichoambulia dhidi ya Yanga, lakini vilevile wakiwa wametoka kufungwa mechi mbili mfululizo za VPL kwa hivi karibuni.

Kwa upande wa Biashara ambao walianza vyema msimu huu, hawajawa na matokeo mazuri lakini katika mechi tano za mwisho, wameshinda moja pekee , sare mbili na vipigo viwili.