Alhamisi , 20th Jul , 2017

Kesi inayowakabili viongozi wa nafasi za juu klabu ya Simba Evans Aveva na Geofrey Nyange 'Kaburu' imehairishwa mpaka Julai 31 ambapo watarudishwa tena mahakamani kusomewa mashtaka yao.

Hata hivyo siku ya leo Geofrey Nyange 'Kaburu' hakuweza kufikishwa Mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mgonjwa amelazwa katika hospitali ya magereza.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya kutakatisha fedha.