Jumanne , 1st Dec , 2020

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Ditram Nchimbi amesema licha ya ushindi mwembamba wanaoupata katika mechi za ligi kuu Tanzania bara, anaamini wapo katika njia nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu. Na jambo muhimu ni kutwaa alama tatu katika kila mchezo.

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Ditram Nchimbi akiwa mazoezini.

Akizungumza na Aast Africa Radio, Nchimbi ameelezea mazingira magumu ya mechi zao za VPL ambazo ameweka wazi kwamba kuna shinikizo kubwa la kufanikiwa msimu huu na ni jambo la kawaida haswa kwa timu za Yanga na Simba.

Nyota huyo anayeichezea timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ameongeza kwamba yeye na wachezaji wenzake wamedhamiria kutwaa ubingwa kwa namna yoyote msimu huu kwakuwa hawana sababu ya kushindwa.

Kuhusu safu ya yao ya ushambuliaji kuonekana kukosa makali, nchini amesema timu inajengwa na kuna presha kubwa ambayo anaamini kuna muda itapungua watakapoanza kufunga mabao.

Vilevile nyota huyo akagusia juu ya mshambuliaji mwenzake, Michael Sarpong ambaye amekua akikosolewa kwa kushindwa kuifungia Yanga mabao kama ilivyotegemewa mwanzoni mwa msimu.

"Ujue sisi wabongo tunajuana wenyewe, Sarpong Michael ni mchezaji mzuri sana, Ila mambo haya huwa yanatokea tu, je mimi nina mechi ya ngapi sijafunga? Lakini nimeshaelewa na ndio maana nacheza hata sifikirii matusi ya wabongo.

Timu zetu hizi mbili zinapresha sana, watanzania ukifanya vzr watakupongeza, ukiharibu watakutukana, Sasa ni yeye Sarpong kujipanga, kutozingatia mambo ya nje, siku akifanya vizuri watamkubali tu na ndio watanzania tulivyo.

Mimi maisha yangu pia ni katika Instagram, najua kilakitu kinachosemwa kuhusu mimi, hivyo ninavyotukanwa, najua Kwakuwa wabongo wanataka nifanye vizuri hakuna kingine.

Hivyo pia watanzania wakumbuke aina ya uchezaji wangu ndio ilivyo, ndivyo nilivyoumbwa, siwezi kuwa mwingine, ninajua nina ubora zaidi na nitatumika vizuri inavyotakikana" Ditram Nchimbi.