Alhamisi , 27th Jul , 2017

Zikiwa zimebakia takribani siku 10 kufungwa kwa dirisha la usajili wa msimu mpya wa  ligi kuu Tanzania Bara, timu ya Mbao FC imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili mchezaji chipukizi Suleiman Kibadeni kutoka Zanzibar kuwatumikia wakata mbao hao kwa

 miaka miwili kuanzia hivi sasa.

Timu hiyo ilinusurika chupu chupu kushuka daraja katika msimu uliyopita ambapo hivi karibuni iliondokewa na nyota wake watano baada ya kuonekana wazuri katika vilabu vingine vya hapa nchini Tanzania.

Wachezaji hao ni makipa Benedict Haule na  Emmanuel Mseja,  kiungo Salmin Hoza waliokwenda Azam FC, beki Jamal Mwambeleko waliokwenda Simba na kiungo Pius Buswita aliyekwenda Yanga.