Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Klabu ya Simba iliendelea kupata ufahari baada ya wachezaji wake 7 kuchaguliwa kwenye kikois bora cha msimu wa 2020-21 cha Ligi Kuu ya Vodacom kwenye usiku wa tuzo za TFF zilizotolewa usiku wa jana.

Baadhi ya wachezaji kutoka Simba na Yanga wakiwa wamepshika tuzo zao baada kuchaguliwa kuingia kwenye kikois bora cha VPL 2020-21.

Wachezaji waliochaguliwa kulingana na ubora waliouonesha msimu mzima na kupewa tuzo ni wafuatao.

Mlinda mlango Aishi Manula (Simba), mlinzi wa kulia Shomari Kapombe (Simba), Mohamed Hussein mlinzi wa kushoto (Simba), walinzi wa kati Joash Onyango (Simba), Dickson Job (Yanga).

Kwa upande wa viungo ni, Mukoko Tonombe (Yanga), Clatous Chama ( Simba) na Feisal Salum (Yanga) ilhali washambuliaji ni John Bocco (Simba, RS Berkaine) aliyeondoka na tuzo ya mfungaji bora wa VPL, Prince Dube (Azam) na Luis Miquissone (Simba, Al Ahly)

Simba imetoa wachezaji 7, Yanga wachezaji 3 wakati Azam imetoa mchezaji 1.