Cesc fabregas anayekipiga kwa sasa Monaco
Si jambo rahisi kwa mchezaji kufikisha mechi nyingi kwa kiasi hichi kwa mchezaji aliyecheza chini ya miaka 20 katika maisha ya soka, Fabregas amefikisha mechi hizo katika mchezo wa mwishoni mwa wiki kati ya timu yake Monaco na Nantes iliyoisa kwa ushindi wa 2-1,lakini hizo mechi zimepatikana katika timu 4 alizopita katika ngazi ya klab ikiwemo Arsenal, Barcelona na Chelsea na sasa Monaco na Timu ya Taifa
Fabregas zao la akademi ya Barcelona ( La Mesia) akiwa pamoja na lionel Messi ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa kiuchezaji akicheza kwenye nafasi ya kiungo mshambuliaji. Pamoja na ushindani alioukuta kwenye timu ya Arsenal kwenye nafasi yake hasa alipokuwepo Patrick Viera ilimchukua muda mchache kupata nafasi na kuwa muhimu katika timu
Hata pia kwa upande wa timu ya Taifa ya Spain alipata upinzani wa nafasi ya moja kwa moja kwa wachezaji wenzie aliokuwa nao pale La Masia kama Xavi Harnandez na Andreas Iniesta
MECHI HIZO 800 ZIMEPATIKANA KWENYE TIMU 4 KWA UWIANO HUU
Arsenal 303
Barcelona 151
Chelsea 198
Spain 38
Pamoja na kushinda vikombe kadhaa akiwa ikiwemo kombe la Ulaya 2008 ,2012 na pia kombe la dunia 2010 Afrika kusini , kwa ngazi ya club ametwa vikombe vingi kwa ligi mbalimbali alizoshiriki