Jumatano , 20th Sep , 2017

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake inacheza mpira mzuri na wakuvutia lakini tatizo imekuwa ni kwa safu ya ulinzi kuruhusu mabao yasiyotarajiwa hivyo kufanya timu yake kupoteza michezo mfululizo.

“Tunacheza mpira wa kuvutia sana tatizo ni moja tu tunashindwa kuzuia kufungwa na wapinzani wetu lakini ndio mchezo wa soka una dakika 90”, amesema Klopp.

Liverpool haijawa na matokeo mazuri siku za hivi karibuni baada ya kupoteza dhidi ya Man City kisha kutoa sare na Sevilla katika mchezo wa UEFA.

Jana Liverpool imeondolewa kwenye michuano ya kombe la ligi EFL Cup na mabingwa wa EPL msimu wa 2014/15 Leicester City kwa mabao 2-0.