Jumanne , 18th Apr , 2017

Jurgen Klopp amesema haitakuwa ajabu kama ataishia kufundisha Liverpool, baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo ya Merseyside.

Jurgen Klopp

Klopp, aliyefundisha klabu mbili za nchini Ujerumani ambazo ni Mainz na Borussia Dortmund, alijiunga na Liverpool Oktoba 2015, na kuongeza mkataba mpya wa miaka 6 kipindi cha kiangazi kilichopita.

Klopp ambaye bado hajaipata taji Liverpool, amesema kusaini kwake mkataba mrefu na klabu hiyo, kunamfanya asiwe na hamu tena ya kutafuta kazi pindi akimalizana na wekundu hao wa Anfield.

Klopp aliliambia gazeti la michezo nchini Ujerumani Sport1: "Sitaziongoza klabu 10 tofauti pindi kazi yangu ya ukocha itakapofika mwisho".

Kuhusu ukame wa mataji wa Liverpool, baada ya miaka 27, ya kukosa ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini, Uingereza, Klopp anakiri kuwa hatasikia furaha pindi atakapomaliza mkataba wake bila ya taji.

"Kama natimiza kazi yangu na Liverpool, kutakuwa na nafasi nzuri, nitashinda kitu hapa.....Nitakuwa katika hali ya huzuni, endapo hatutoshinda kitu. Watu wanatarajia Liverpool kushinda mataji".