Alhamisi , 18th Mei , 2017

Kocha msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangalu amesema, kikosi chake kipo imara kupambana na Azama FC mwishoni mwa juma hili huku akidai watapambana kuhakikisha wanabakia katika nafasi ya tatu ndani ya msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo amesema japokuwa ligi imekuwa ngumu lakini wanamatumaini makubwa ya kuwafunga wapinzani wao Azam FC waliowatangulia nafasi moja mbele katika msimamo wa ligi.

"Tunacheza na Azam FC katika uwanja wao...Wachezaji wangu wote kiafya wapo vizuri, tangu tumeanza Ligi tumekuwa washindani mpaka hii leo tupo nafasi ya nne tukiwa tumepishana pointi mbili na wapinzani wetu Azam FC ambao wapo nafasi ya tatu na tunataka tushindane ili tuipate nafasi ya tatu. Hata mwakani tujipange upya tuwe katika ushindani wa kuwania Ubingwa". Alisema Jangalu

Pamoja na hayo kocha huyo amewataka waamuzi wa michezo kuchezesha mechi hizo za mwisho kwa kufuata sheria zote za Soka ili kuhakikisha mshindi anapatikana kihalali katika kila mchezo.