Jumapili , 17th Sep , 2017

Dereva wa timu ya Mercedes Lewis Hamiliton ameongeza wigo wa alama kati yake na mpenzi wake Sebastian Vettel wa Ferrari baada ya kuongoza kwenye mbio za jioni ya leo Singapore Grand Prix.

Hamiliton ameongoza mbio hizo mwanzoni kabisa baada ya Sebastian Vettel kugongana na dereva mwenzake wa Ferrari Kimi Raikkonen pamoja na Max Verstappen wa Red Bull na kumuacha Hamiliton akiongoza mbio hizo hadi mwisho.

Sebastian Vettel na wenzake walijitoa baada ya kugongana hivyo inawabidi wasubiri mbio zinazokuja ili kuona kama wanaweza kumpiku Hamiliton.

Mbio za leo za SingaporeGP zimefanyika usiku kwa mara ya kwanza katika historia ya Formula1. Lewis Hamiliton sasa amejiongezea pointi 25 ambazo zinamfanya kufikisha pointi 263 dhidi ya 235 za Sebastian Vettel.