Jumamosi , 17th Jun , 2017

Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm, ametoa ushauri wake na kusema Simba wanafanya makosa kumuacha golikipa Daniel Agyei.

Hans amesema Agyei ni kipa ambaye amewapa mafanikio makubwa Simba ikiwemo kombe la FA na fainali ya Kombe la Mapinduzi na ni kati ya makipa waliofanya vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom licha ya ugeni wake.

Simba huenda watamuacha kijana huyo raia wa Ghana kwa kuwa imewasajili Aishi Manula kutoka Azam FC na Emmanuel Mseja wa Mbao FC.