Jumapili , 13th Aug , 2017

Mchezaji wa mashetani wekundu kutoka Old Traford Manchester United, Romelo Lukaku leo ameonyesha kuwa yeye sio wa mchezo mchezo baada ya kuwanyoosha West Ham mapema sana kwa kuwatandika goli 2 mfululizo miongoni mwa magoli manne waliyofungwa na Man U

Mchezaji Romelo Lukaku akishangilia goli

Lukaku aliwapa heshima Man U dakika ya 33 alipowatundika West Ham goli la kwanza, na baada ya dakika 19 tu tangu awafunge goli hilo, aliwapa lingine bila kuwaangalia usoni ikiwa ni dakika ya 52.

Baada ya Mourinho kuusoma mchezo alimtoa Rashford dakika ya 79 ya mchezo na kumuingiza serengeti boy Anthony Martial uwanjani, na ndani ya dakika 8 alizozisakata kabumbu alifanikiwa kuiandikia Man U goli la 3 katika dakika ya 87.

Kama haikutosha mtu mweusi Paul Pogba aligoma kutoka uwanjani hapo bila kuandika historia, na kuwatundika goli la 4 West Ham katika dakika ya 90, iliyoipa ushindi wa kiume timu ya mashetani wekundu Manchester United.

Baada ya mchezo huo Romelo Lukaku alikaririwa akisema "unapoichezea Manchester United una kazi ya kufanya, na yangu ni kufunga magoli", alisema Lukaku.

Ushindi huo wa leo unaiweka timu ya Manchester United kwenye nafasi ya kwanza kwa kuwa na poinnt 3 na goli 4 mkononi, huku ikifuatiwa na Huddersfield yenye point 3 na goli 3 mkononi.