Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Kocha msaidizi wa Simba SC Selemani Matola amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa kundi A wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi Al Ahly Misri mchezo utakao chezwa kesho jijini Dar es salaam, wakati nahodha John Bocco anaimani mbizu za benchi la ufundi zitawapa ushindi kesho.

Makocha wa Simba SC

Wekundu wa msimbazi watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi na wakihistoria wa klabu bingwa frika Al Ahly katika dimba la Benjamini Mkapa Dar es salaam, mchezo utakao chezwa majira ya Saa 10:00 jioni.

''Sio mechi rahisi ni mechi ngumu ukichukulia kwamba tulipata matokeo katika mchezo uliopita lakini sio mechi rahisi ni mechi ngumu na ukiangalia ligi hii ni ligi ya mabingwa hakuna mtu mrahisi yani. Lakini tumejipanga pamoja na kwamba tunakutana na timu ambayo ni nzuri na iko bora zaidi lakini lazima tuhakikishe tunapata matokei katika mchezo wetu wa nyumbani hapo kesho.''

Kwa upande wa nahodha wa kikosi Simba John Bocco amesema wao kama wachezaji wapejipanga vizuri na wanaimani mbiznu za benchi lao la ufundi zitawawezesha kushinda mchezo huo.

''tumejipanga vizuri tunaamini tutaenda kucheza mchezo wetu wa kesho tukiwa katika morari nzuri na nia nzuri ya kuweza kushinda huu mchezo tunaenda kumalizia mazoezi yetu ya mwisho leo na walimu wetu tunaamini watatutpa mbinu nzuri.''

Tunaheshimu wapinzani ni timu kubwa, kwani ni timu yenye uzoefu mkubwa katika haya mashindano pia ni timu kubwa kwa Afrika tunawaheshimu kwa hilo lalini tunaamini kwa mbinu tutakazo ingia nazo kesho kutoka kwa walimu wetu tutaweza kufanikiwa kushinda.''

 

Al Ahly ndio vinara wa kundi hili wakiwa na alama 3 sawa na Simba ambao wapo nafasi ya pili, Ahly wakiwa kileleni kwa faida ya mabao mengi ya kufunga. As vita wanashika nafasi ya 3 na Al Merrick wanaburuza mkia.