Malinzi na Mwesigwa mambo yazidi kukwama

Monday , 17th Jul , 2017

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamerudishwa rumande kwa mara nyingine kutokana na upelelezi  wa kesi yao kutokamilika hivyo wamerudishwa tena Mahakamani Julai 31

 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea mpaka sasa.

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa na matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 yakiwemo kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

Recent Posts

Kiungo Papy Kabamba Tshimbi mwenye jezi nyekundu ambaye anatarajiwa kutua Yanga wakati wowote.

Sport
Yanga kumnasa mchezaji wa Swiziland

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Current Affairs
Ndugai ameridhia kufukuzwa wabunge 8 CUF

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla

Current Affairs
Madaktari bingwa China kuhudumia Tabora