Jumatatu , 18th Sep , 2017

Mabingwa watetezi wa ligi ya Mabingwa Afrika Mamelodi Sundowns, wamejiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa msimu wa pili mfululizo.

Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Mamelodi Sundowns wameshinda mchezo wao wa robo fainali mkondo wa kwanza dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco. Bao pekee la mshambuliaji Yannick Zakr raia wa Ivory Coast limeipa Mamelodi ushindi wa 1-0 na sasa watasubiri mchezo wa marejeano jumamosi ijayo nchini Morocco.

Katika robo fainali nyingine iliyopigwa nchini Lyibya kati ya wenyeji Al Ahli dhidi ya Etoile du Sahel.ya Tunisia ilimalizika kwa sare tasa ya 0-0 na kufanya kazi iwe nyepesi kwa klabu ya zamani ya Emmanuel Okwi Etoile du Sahel. kwenye mchezo wa marejeano.