Alhamisi , 19th Jan , 2017

Timu ya Manchester United imepata kipato kikubwa kuliko timu yoyote katika msimu uliopita na kuipiku Real Madrid iliyokuwa kinara kwa mapato kwa takriban miaka 11

Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni ya Deloitte ambayo ni miongoni mwa kampuni kubwa za ukaguzi duniani ambapo imeitaja Man United kuingiza paund milioni 515 (euro 689m) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 1.6 katika msimu wa 2015/16

Hii ni mara ya kwanza kwa Man United kushikia nafasi hiyo tangu msimu wa 2003/04.

Katika taarifa hiyo, klabu hiyo ya Man United inayoshiriki ligi kuu ya England ( EPL) imeshuhudia mapato yake yakiongezeka kwa wastani wa paund milioni 71 (euro milioni 100) na kwa kiasi kikubwa ni mapato ya kibiashara.

Real Madrid waliokuwa vinara wameengiza paund milioni 463 (euro 620.1) sawa na shilingi trilioni 1.478 wameporomoka hadi nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona walioendelea kubaki katika nafasi ya pili kwa kipato chao cha shilingi za kitanzania trilioni 1.479

Bayern Munich imepanda kutoka nafasi ya 5 hadi ya nne, huku Man City pia wakipanda kutoka nafasi ya sita hadi ya 5.

Ukijumlisha vipato vya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia paund bilioni 6.41 (euro billioni 7.4) sawa na shilingi 17.7 za kitanzania kikiwa ni kiwango ambacho hakijawahi kutokea.