Jumatatu , 22nd Mei , 2017

Msemaji wa Klabu ya Simba aliyefungiwa na TFF, Haji Manara amefunguka mengine mapya kwa kudai bado hajakubaliana na ubingwa wa ligi kuu Tanzania walioutwaa Yanga SC na kudai kuwa wao (Simba SC) ndiyo mabingwa wa ligi hiyo msimu huu.

Haji Manara

Manara amebainisha hayo kupitia mitandao ya kijamii kwa kurusha vijembe kwa wapinzani wao wa jadi na kudai kwamba kama Serengeti Boys waliweza kushinda rufaa yao na kuweza kushiriki michuano ya vijana huko nchini Gabon basi nao watashinda bila shika.

"Wabongo bana kwa 'double standard' hawajambo, Serengeti Boys walikuwa Gabon kwa kushinda rufaa ila Simba hawastahili....Mjiandae kiakili Gongowazi, Simba ndiyo 'champion' msimu huu". Ameandika Manara

Tayari Simba imewasilisha malalamiko yao kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) wakipinga kupokwa pointi 3 na TFF baada ya kupewa na bodi ya ligi kutokana na Kagera Sugar kumtumia mchezaji asiyestahili katika mechi dhidi yao, ambapo Kagera Sugar ilipata ushindi wa mabao 2-1.