Jumanne , 5th Jul , 2022

Afisa habari wa Yanga Haji Manara amemuomba msamaha Rais wa TFF Wallace Karia kutokana na tukio lililotokea Jijini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Sunday Manara

Mara baada ya mchezo huo kuna video iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha Afisa huyo wa Yanga akijibizana au kutupiana maneno na Rais wa TFF Wallace Karia huku wengi wakitafsiri kuwa Manara alikuwa akimtukana Rais huyo.

Akiongea na waandishi wa habari  Manara amesema kuwa alikosea kujibizana na Rais hadharani huku akiweka wazi kuwa yupo tayari kuwajibishwa iwapo itaonekana. Inastahili.

''Jana nilienda kumuona rais wa TFF nyumbani kwake,  kumuomba radhi juu ya kilichotokea naamini mimi nikama mwanae natumaini atakuwa amenielewa"amesema Haji Manara.