Jumatano , 18th Oct , 2017

Kocha wa Napoli Maurizio Sarri amesema klabu ya Manchester City ina uwezo wa kutwaa ubingwa wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Sarri amekisifu kikosi hicho cha Pep Guardiola baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa kundi F jana usiku ambapo timu yake ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa matajiri hao wa jiji la Manchester City.

"Ni timu nzuri, ina muunganiko na inacheza soka la kuvutia lenye mbinu nyingi, kwa ubora wao wanayo nafasi ya kuwa mabingwa”, amesema Sarri.

Naye kocha wa Manchesterr City Pep Guardiola alikisifu kikosi cha Maurizio Sarri kuwa kina vijana wengi wanaojua kucheza soka na kuwa ndio timu ambayo imempa changamoto kubwa msimu huu.

“Ni timu yenye vijana wengi wanaojua kucheza soka na wanajituma kweli kutafuta matokeo, ni timu bora na inaweza kuitoa Juventus kwenye ufalme wa soka la Italia”, amesema Guardiola.