Jumatano , 18th Oct , 2017

Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kuachana na kocha wake msaidizi Jackson Mayanja leo baada ya tetesi za muda mrefu.

Kupitia kwa Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wameachana na kocha huyo kwa uungwana bila matatizo kwani ana mambo yake binafsi ambayo anahitaji muda zaidi wa kuyashughulikia.

Manara ameweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye maneno haya, “Yes Tumemalizana na kocha Mayanja kiungwana,,,angalia video hyo,,Thanks kocha Jack,,kila la kheri ,,we gonna mic u Sir”.

Mayanja mwenyewe amefunguka kuwa anaishukuru klabu na uongozi mzima kwa muda wote ambao wamefanyakazi pamoja lakini pia kumruhusu akashughulikie matatizo yake nyumbani kwao Uganda.

Tazama video hapa Mayanja akieleza sababu za kuachana na Simba.