Jumamosi , 19th Aug , 2017

Wakati mabingwa wa Kombe la FA, Simba wakilazimishwa suluhu dhidi ya Mlandege ya Zanzibar katika mechi ya kirafiki iliyofanyika juzi usiku.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amewaodoa hofu mashabiki baada ya timu yao kushindwa kupata ushindi katika mchezo huo. 

Mayanja amesema kiufundi mchezo huo umewasaidia kuendelea kuwafahamu wachezaji wao na matokeo ya sare yaliyopatikana yamesababishwa nyota wao kucheza kwa tahadhari.

"Ni kweli suala la ushambuliaji na umaliziaji halijakaa vizuri kwa upande wa timu yetu, ila ninawaondoa hofu mashabiki na wanachama wa Simba, tuko vizuri na watatuona tukirejea Dar es Salaam," alisema kocha huyo.

Leo usiku Simba inatarajiwa kushuka tena dimbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gulion, mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Amaan.