Ijumaa , 12th Sep , 2014

Timu ya soka ya Mbeya city jumamosi hii inatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya Vipers Fc zamani bunamwanya inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uganda mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya sokoine Mbeya.

Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten amesema kuwa kikosi hicho kinataraji kutua jijini Mbeya ijumaa ya kesho kikiwa na msafara wa watu 25 viongozi 5 na wachezaji 20.

Ten ameongeza kuwa timu hiyo ianataraji kuwa kipimo kizuri kwa timu ya Mbeya City kwani mmoja ya timu amabazo zimeonyesha uwezo mkubwa katika ligi ya Uganda na kufanikiwa kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya nchi hiyo.

Huu utakuwa mchezo wa mwisho wa kujipama nguvu kwa Mbeya City kabla kuanza mbilinge la ligi kuu ya soka Tanzania bara inayotaraji kuanza kutimua vumbi September 20 kwenye viwanja mbalimbali.

Mbeya city ambayo ilikamata nafasi ya tatu msimu uliopita kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara inaendelea na mawindo yake chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi na msaidizi wake Suleiman Jabir

Afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten amewaomba wakazi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo jumapili kuishuhudia timu yao pendwa ikionyesha kile ambacho imejipanga nacho kwa ajili ya ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014/2015.