Jumatano , 16th Aug , 2017

Timu ya Mchenga BBall Stars imepata kipigo cha pointi 87-78 dhidi ya wapinzani wao TMT katika mechi ya pili ya fainali ya Sprite BBall Kings iliyofanyikia leo katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam Jioni ya leo.

Kutokana na ushindi huo timu ya TMT imeweza kurudisha heshima kwa mashabiki wake waliyoweza kufika kuwatazama baada ya kufungwa katika mechi ya ufunguzi ya fainali hizi.

Pamoja na hayo, timu ya Mchenga BBall Stars leo ilionekana kucheza chini ya kiwango chake ambacho kimezoeleka kuonekana kila wawapo uwanjani jambo ambalo baadhi ya mashabiki kufikiri pengine wameamua kuwaachia wapinzani wao nao waweze kushinda mchezo wa leo.

Kwa upande mwingine, TMT na Mchenga BBall Stars watakutana tena siku ya Jumamosi ili kuweza kucheza 'game 3' ya fainali hizi ambapo mpaka sasa timu zote mbili zimeweza kupoteza mchezo mmoja mmoja na kupata mmoja mmoja.