Jumamosi , 20th Mei , 2017

Mechi 8 za funga dimba ya ligi kuu Tanzania Bara zinapigwa leo nchi nzima huku vita kuu ikiwa ni kwenye mechi 6 zitakazoamua timu 3 za kushuka daraja msimu huu.

Timu zilizo hatarini kushuka daraja

Timu zilizokatika wakati mgumu na zinahitaji ushindi wa hali na mali ni Mbao FC, Toto African, Majimaji FC, Ndanda FC na African Lyon wakati JKT ikiwa imekwisha tangualia 'kaburini'

Mechi 5 zitakazotolewa macho na wengi ni ile ya Mbao FC dhidi ya Yanga itakayopigwa katika dimba la CCM Kirumba Mwanza, ambapo Mbao FC inahitaji ushindi pekee ili iweze kusalia ligi kuu Tanzania Bara wakati Yanga wakisaka heshima ikiwa ni pamoja na kulipiza kisasi cha kuvuliwa ubingwa wa FA na timu hiyo.

Mechi nyingine zinazohusisha timu zinazosaka kujinasua ni pamoja na Tanzania Prisons dhidi ya African Lyon ambapo African Lyon ndiyo iliyo kwenye nafasi mbaya zaidi, Ndanda FC nayo itakuwa ikiitumia JKT Ruvu ambayo tayari imeshuka daraja ili kujinasua.

Mechi nyingine itakayotolewa machi na wengine ni ile ya Majimaji dhidi ya Mbeya City ambapo Majimaji iko katika wakati mgumu na inahitaji ushindi ili isalie katika ligi hii.

Timu yenye hali mbaya zaidi ni Toto African ambayo itakuwa Manungu kumaliza na Mtibwa Sugar. Toto licha ya kusaka ushindi, pia itakuwa ikiwaombea washindani wake katika nafasi za chini wafanye vibaya ili ushindi wake uwe na manufaa. 

Ligi hiyo inahitimishwa huku tayari machampioni watetezi Yanga wakiwa na asilimia 99 za ubingwa kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, licha ya kuwa na point 3 mbele ya washindani wao katika ligi ya msimu huu, Simba SC.

Mechi zitakazopigwa leo ambazo ni za mzunguko wa 30, ni hizi...