Alhamisi , 30th Jun , 2022

Bondia mtanzania Mfaume Mfaume atapanda ulingoni kesho kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili kuwania ubingwa wa WBF Afrika uzito wa Welterwight dhidi ya Bondia kutoka Misri Abdulmonem Said. Pambano litakalofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam kuanzia majira ya Saa 12 jioni.

Mfaume Mfaume anapanda ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya miaka 2

Mfaume Mfaume amesema amejiandaa vizuri kuelekea Pambano hili na amewaahidi watanzania kupata ushindi hapo kesho kutoka na maandalizi mazuri aliyoyafanya.

“Nimepata maandalizi ya muda mrefu kwa hiyo watanzania watarajie kuona ngumi Biriani kesho kwa uwezo wa Mungu watanzania watafurahi, kwa sababu ushindi wa Mfaume Mfaume ni ushindi wa Tanzania” Ameseme Mfaume

Kabla ya pambano hili yatafanyika mapambano mengine saba ya utangulizi ambapo Mwana dada Stumai Muki atacheza dhidi ya Chimwemwe Banda wa Malawi, Laurent Segu ataminyana na Thomas Mahaule, Pius Mpenda atazichana na George Dimoso, Issa Nampepeche dhidi ya Juma Choki, Oscar Richard anacheza na Bongani Makovora kutoka Zimbabwe, Hamisi Maya atanyukana na Murdochee Katembo wa Congo na Ibrahim Class atazichapa na Peter Pambeni wa Zimbabwe.