Jumamosi , 14th Jan , 2017

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2017 maarufu kama AFCON inaanza leo Jumamosi nchini Gabon huku waandalizi hao Gabon wakikabiliana na Guinea-Bissau.

Mchezo mwingine utakayochezwa leo katika michuano hiyo ni pamoja na mechi kati ya Burkina Faso na Cameroon usiku wa saa nne.

Katika kipindi cha siku 23 timu 16 zitachuana kuwania kombe hilo lenye umaarufu mkubwa Afrika.

Michuano hiyo ilitarajiwa kufanyika nchini Libya, lakini kutokana na misukosuko ya kuvunjika kwa amani iliwalazimu wasimamizi kubadili nia na kuelekea Gabon ambayo iliandaa michuano hiyo mwaka 2012.

Algeria na Zimbabwe zitakutana kesho majira ya saa moja usiku na usiku wa saa nne Tunisia itakutana na Senegal