Ijumaa , 21st Nov , 2014

Mkutano mkuu wa dharura wa Chama cha Mpira wa Kikapu mkoani Dar es salaam BD,unatarajiwa kufanyika kesho kwa kushirikisha viongozi wa Timu shiriki za Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio,Makamu wa Rais wa BD,Richard Julles amesema lengo hasa ni kutathimi Ligi ya mkoa ili kuweza kujua upungufu uliopo na kutafutia ufunguzi ili kuweza kuboresha Ligi hiyo.

Julles amesema pamoja na tathimini ya Ligi hiyo,watajadili mipango ya mwaka ujao ya chama ili kuweza kupata maoni mbalimbali kutoka kwa wanachama ili kuweza kufikia malengo ya chama waliyojipangia.