Jumamosi , 21st Oct , 2017

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amekanusha taarifa za kuwa maneno yake aliyosema kuhusu makocha wanaolia yalikuwa yanamlenga kocha wa Chelsea Antonio Conte.

Meneja huyo raia wa Ureno amesisitiza kuwa hakumlenga Antonio Conte aliposema kuwa hafurahishwi na makocha wanaolia kuwa na majeruhi kwenye timu zao.

Wawili hao wamekuwa na majibizano siku za hivi karibuni lakini Mourinho amesema hana ugomvi na kocha huyo labda kama yeye anashida binafsi na Mreno huyo.

"Sizungumzi naye, sijui kwa nini anaongea na mimi lakini sio shida au labda si kosa lake ni kosa la waandishi wa habari wanapompa ujumbe usio sahihi," amesema Mourinho.