Jumatatu , 20th Nov , 2017

Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar imesema itapandisha vijana wa timu B endapo kocha Zuberi Katwila atahitaji kusajili wakati huu wa dirisha dogo.

Akiongea na eatv.tv msemaji wa timu hiyo Thobias Kifaru amesema kuw akikosi chao bado ni imara na kimekamilika katika maeneo yote kuanzia ulinzi hadi ushambualiaji.

“Tuna kikosi kilicho bora, tuna walinzi bora, tuna washambuliaji bora, tuna viungo bora na magolikipa bora lakini ikitokea pengo tuna vijana wameshapta ukomavu kwenye timu B hivyo tutawapandisha”, amesema Kifaru.

Mtibwa Sugar jana ilikubali kichapo cha bao 1-0 kwenye uwanja wake nyumbani Manungu kutoka kwa Kagera Sugar. Baada ya matokeo hayo Mtibwa inashika nafasi ya 4 ikiwa na alama 17.

Dirisha dogo la usajili limefunguliwa Novemba 15 na litafungwa Desemba 15 ambapo vilabu vya ligi kuu vitaboresha vikosi vyao.