Jumatatu , 27th Mar , 2017

Kiungo mshambuliaji kutoka timu ya Taifa Stars, Saimon Msuva amesema mechi inayotarajiwa kuchezwa Jumanne (kesho) dhidi ya Burundi itakuwa kali zaidi kwa sababu wanataka kufuta historia ya kufungwa na timu hiyo.

Saimon Msuva

Mshambuliaji huyo amesema walikuwa hawajuani vizuri na kikosi hicho ndiyo maana ilipelekea wao kuwekwa katika rekodi ya kufungwa mara zote mbili walipokutana nao.

“Unajua Burundi tumecheza nao mara mbili na zote wametufunga, kwa hiyo tunataka tulipize kisasi, Hawa Botswana tulikuwa tunacheza nao hatujuani vizuri, lakini Burundi tunajuana sana kwa hiyo mechi itakuwa ngumu sana,” Alisema Msuva

Pamoja na hayo kiungo huyo alionesha hali ya wasiwasi juu ya mchezaji Laudit Mavugo kutokana na uzuri wake na kusema atawasumbua katika mchezo huo.