Jumanne , 18th Apr , 2017

Mwamuzi Mtanzania Frank John Komba ni miongoni mwa waamuzi walioorodheshwa kuchezesha michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17 Africa Cup of Nations), michuano ambayo imepangwa kufanyika nchini Gabon.

Komba yupo kwenye orodha ya waamuzi wasaidizi (Assistant Referees au washika kibendera) na ni mwamuzi pekee kutoka Tanzania aliyepata fursa hiyo.

Komba anaungana na waamuzi wengine wawili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki Pacifique Ndabihawenimana (mwamuzi wa kati kutoka Burundi) na Davies Ogenche Omweno (mwamuzi wa kati kutoka Kenya).

Hii ni habari njema kwa soka la Tanzania ambapo wadau wamekuwa wakipaza sauti zao kutaka wachezaji wa Tanzania kujituma ili kupata fursa ya kucheza nje lakini pia wamekuwa wakihoji kwa nini makocha wengi wazawa hawapati nafasi za kufundisha timu nje ya nchi hali kadhalika kwa waamuzi wa nyumbani wamekuwa hawapati mechi za kutosha za kimataifa licha ya kuwa na beji za FIFA.

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ ni miongoni mwa timu ambazo zitashiriki katika michuano hiyo ambayo inatarajia kuanza Mei 14 mwaka huu.

Hii ndiyo orodha ya waamuzi