Jumatatu , 24th Jul , 2017

Klabu ya Mtibwa Sugar yenye makao makuu yake Turiani mkoani Morogoro imefanikiwa kunasa saini ya kiungo mkongwe wa kutokea JKT Ruvu, Hassan Dilunga kuitumikia timu hiyo kwa kandarasi ya miaka miwili katika msimu mpya wa ligi kuu 2017/2018

Mchezaji mpya wa Mtibwa Sugar Hassan Dilunga.

unaotarajiwa kuanza muda si mwingi.

Kusajiliwa kwa Dilunga kunafanya idadi ya nyota wapya katika kikosi hicho kufikia sita (6) mpaka sasa baada ya usajili wa awali wa Hussein Idd kutoka Oljoro JKT anayemudu kucheza beki ya kati, Seleman Kihimbi “Chuji”  kutoka Polisi Moro, Salum Kupela Kanoni kutoka Mwadui, Shaban Kado kutoka Mwadui na Rifat Khamis kutoka Ndanda FC.

Mara baada ya usajili huo, Dilunga amesema Mtibwa ndiyo mahala sahihi kwake na ndiyo sababu ya yeye kukataa ofa nyingi alizopata kutoka katika vilabu vingine.

“Nafikiri nimekuja mahala sahihi, nimepata ofa nyingi sana lakini nilipoona Mtibwa Sugar wananihitaji sikutaka kufikiria mara mbili maana nilikuwa natamani kuichezea klabu hii, namshukuru Allah kwa kunifikisha mahala hapa nadhani patakuwa sahihi sana kwangu", amesema Dilunga.

Kwa upande mwingine, Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), limesema mpaka sasa ni timu mbili, kati ya 62 ndizo zimefanya usajili hivyo imetoa tahadhari kwa klabu zote zilizopo nchini kuendelea kufanya usajili katika siku 12 zilizobakia kabla ya kufungwa dirisha la usajili kwa kuwa mwaka huu hawataweza kuongeza siku kama walivyofanya mwaka uliyopita katika usajili.