Alhamisi , 8th Dec , 2016

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo amemkabidhi Mwamuzi kutoka Tanzania Jonasia Rukyaa funguo ya gari alilozawadiwa kwa kuchezesha vizuri katika fainali za wanawake barani Afrika, zilizofanyika nchini Cameroon hivi karibuni.

Jonasia akikabidhiwa funguo na Rais Malinzi

Taarifa ya TFF imesema kuwa wadau kadhaa wa mpira wa miguu, wamemzawadia gari Jonesia Rukyaa mwamuzi mwandamizi wa FIFA ambaye alipangwa kuchezesha michuano hiyo iliyomalizika kwa timu ya wanawake ya Nigeria kuibuka na ubingwa.

Jonesia, ambaye amepata pia kuchezesha mchezo wa watani wa jadi katika soka nchini, alichezesha mechi ya awali na kuonekana kutokuwa na upungufu kwenye kutafsiri sheria 17 za soka.

Alipangwa kuchezesha mechi ya mshindi wa tatu kati ya Ghana na Afrika Kusini.

Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) akimkabidhi zawadi mwamuzi Jonasia Rukyaa