Jumatatu , 29th Mei , 2017

Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, amemtaka mshambuliaji wa timu hiyo, Mzimbabwe, Donald Ngoma, asiwayumbishe kwa chochote, na kama amepanga kuondoka kwenye timu hiyo anaweza kufanya hivyo kwani wapo watakaoziba nafasi yake.

Mzee Akilimali amesema hayo baada ya mshambuliaji huyo kudaiwa kuonesha vitendo vya utovu wa nidhamu ndani ya timu ikiwemo ya kususia kusafiri na wenzake kwa madai ya kutolipwa mshahara wake katika.

“Ninachokifahamu ni kwamba, bado ana mkataba na Yanga, ingawa nilimsikia kwamba hana mpango wa kuondoka na anafurahia kuwepo katika timu yetu, lakini kwa haya mambo ambayo anazidi kuyafanya ni vyema akaenda anapotaka...Kitu kizuri ni kufuata taratibu na sheria zipo lakini si kuendelea kufanya vitendo viovu, maana hajazuiwa kuondoka kwa sababu yeye siyo wa kwanza kucheza Yanga, tunathamini mchango wake ila ni bora akaenda anapotaka kwani tunaamini wapo watakaoingia kuziba nafasi yake” alisema Mzee Akilimali