Jumanne , 27th Sep , 2016

Nchi sita kati ya 11 zinatarajia kushiriki mashindano ya kanda ya tano ya mpira wa kikapu yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba mosi mpaka saba mwaka huu katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi ya Kikapu, katika uwanja wa ndani wa Taifa

Kamishna wa ufundi na mipango wa chama cha mpira wa kikapu nchini TBF Manase Zabroni amesema, waamuzi wa mashindano hayo wameshachaguliwa na Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) na wageni wote wanatarajiwa kuanza kuwasili nchini kuanzia Septemba 30 mwaka huu tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

Manase amezitaja nchi zilizohakiki kushiriki mashindano hayo kuwa ni Rwanda, Burundi, Sudani Kusini, Kenya, Somalia na wenyeji Tanzania.