Jumanne , 21st Feb , 2017

Mchezaji wa Barcelona Neymar na klabu yake watasimama mahakamani katika kujibu mashtaka ya uhamisho wa mchezaji huyo, kutoka klabu ya Santos, baada ya kushindwa rufaa.

Neymar

Kesi hiyo inaihusu kampuni ya uwekezaji ya Brazil DIS, inayomiliki asilimia 45 ya mauzo ya Mbrazil huyo,imelalamika kuwa ilipewa kiasi kidogo cha fedha, wakati Neymar alipouzwa Barcelona kutoka Santos, kwa ada ya £49 mwaka  2013.

Klabu ya Santos, Neymar, Mama yake na kampuni inayomilikwa na wazazi wake, watafikishwa mahakamani.

"Santos FC, Barcelona FC, Neymar, mama yake Nadine Goncalves na N&N, kampuni ya familia, wamepoteza rufaa yao, ya kukataa rushwa na ufujaji," Taarifa ya mahakama kuu ya Hispania, ilisema.

Neymar anaweza kukumbwa na kifungo cha miaka miwili jela na faini ya paundi milioni 8, endapo atapatikana na hatia.

Lakini kwa mujibu wa sheria za Hispania, kifungo chini ya miaka miwili hutolewa na kubaki faini peke yake.