Alhamisi , 15th Apr , 2021

Klabu ya Manchester United ya England inatazamiwa kuwakosa nyota wake kadhaa wa kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali watakaposhuka dimbasaa 4:00 usiku wa leo Aprili 14,2021 kucheza dhidi ya Granada kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya ligi ya Europa.

Nahodha na mlinzi wa Manchester United, Harry Maguire (kushoto) na mshambuliaji Marcus Rashford (kulia).

Wachezaji watakaokosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kuoneshwa kadi za njano mfululizo ni kiungo Scott McTominay, walinzi, Luke Shaw na Harry Maguire huku mshambuliji wake tegemezi, Marcus Rashford akiwa na hati hati ilhali Erick Bailly anasumbuliwa na Covid-19.

Kwa upande wa Granda, wao watawakosa Domingos Duarte, Yan Etek kutpokana na kuoneshwa kadi za njano mfululizo huku Luis Milla n aNeyder Lozano wakiwa na majeraha.

Manchester United yupo mbele kwa mabao 2-0 baada ya ushindi huo kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hivyo ushindi au sare ya aina yeyote itamfanya afuzu kwenda hatua ya nusu fainali huku Granada akihitaji ushindi wa utofauti wa mabao matatu ili kutinga nusu fainali ya ligi ya Europa.