Jumamosi , 24th Sep , 2016

Bingwa wa masumbwi ya uzani mzito kutoka Uingereza Tyson Fury ameahirisha pambano lake na Wladimir Klitschko kwa mara ya pili kwa sababu ya afya yake kuwa katika hatihati.

Wladimir Klitschko na Tyson Fury

Ingawa mapromota wa bondia huyo hawakufichua taarifa zaidi lakini wamesema "Hali yake ni mbaya mno na haimruhusu kushiriki pambano hilo la maruduiano".

Fury, mwenye umri wa miaka 28, alimshinda Klitschko kutoka Ukraine kwa pointi katika pambano la kwanza mnamo Novemba mwaka jana.

Pambano la marudiano la awali lilipangwa Julai 9 katika uwanja wa Manchester Arena, na liliahirishwa hadi Juni baada ya Fury kuvunjika fupa la kisigino chake huku Pambano jipya la marejeo lilipangwa kufanyika Oktoba 29.